Klabu ya Azam Fc ndio mabingwa wapya wa kombe la Mapinduzi wakifanikiwa kuwafunga Simba Sc goli moja.
Goli la Azam lilifanikiwa kufungwa na kiungo mkabaji Himid Mao Ninja katika kipindi cha kwanza.
Goli ilo la Himid lilidumu paka dakika 90 kumalizika na Azam kufanikiwa kuondoka na kombe.
Katika mchezo huo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Alli Mohamedi Shein.
Baada ya ushindi huo Azam watakuwa wamechukua kombe la mapinduzi kwa mara ya 3.
Katika michuone hii Azam ndio timu pekee ambayo haukuruhusu goli.








Maoni
Chapisha Maoni